Gari la muimbaji Miley Cyrus lililoibiwa baada ya majambazi kuvamia nyumba yake ya Los Angeles limepatikana.

Kwa mujibu wa TMZ kuna mtu aliliona gari hilo lenye thamani ya
milioni 218 likiwa limeegeshwa mtaani na kuwapigia simu maaskari.
Inasemekana gari hilo halijaharibika na inahisiwa huenda majambazi
waliogopa na kuamua kulitelekezwa baada ya kuona habari zimesambaa za
kuibiwa kwake.
Miley Cyrus alikuwa nchini Sweden kwenye ziara ya Bangerz wakati majambazi wanavamia nyumba yake.
Post a Comment