Kwa siku za hivi karibuni wasanii wengi wakubwa wa Marekani
wamejifungua huku wengine wakiripotiwa kuwa wajawazito wanaotegemea kuwa
na mtoto wa kwanza.

Member wa zamani wa Destiny’s Child, Kelly Rowland Jumanne ya wiki
hii ametangaza kuwa mja mzito kupitia Instagram, na kupost picha ya pea
mbili za viatu aina ya Jordan kimoja cha wakubwa na kingine cha watoto.
“I’ll be stuntin like my daddy.” Aliandika.

Ingawa hakusema moja kwa moja kuwa ni mjamzito, mtu wake wa karibu
aliiambia US Weekly kuwa kweli Kelly ana ujauzito wa miezi miwili.
Huyo atakuwa mtoto wa kwanza wa Kelly Rowland kwa mume wake Tim Withernspoon
Post a Comment