Ufunguzi rasmi wa fainali za kombe la dunia nchini Brazil
unatarajiwa kufanyika kesho Alhamisi (June 12), na Jennifer Lopez
anatarajiwa kuungana na rapper Pitbull pamoja na Claudia Leitte
kutumbuiza wimbo rasmi wa kombe la dunia katika sherehe hizo.

Pamoja na FIFA mapema wiki hii kutangaza kuwa Lopez asingetumbuiza
katika ufunguzi huo, muwakilishi wake amethibitisha uwepo wake kwa
PEOPLE, kwa mujibu wa Aceshowbiz.
“Jennifer has always wanted to participate in the World Cup
opening ceremonies, we have been trying to work out scheduling and
logistics. Any statements to the contrary were premature. Jennifer would
not want to disappoint her fans or fans of futbol. She will be there.” Alisema muwakilishili huyo.
J’Lo rapper Pitbull na muimbaji wa Brazil Claudia Leitte
wameshirikiana katika wimbo rasmi wa kombe la dunia mwaka huu uitwao ‘We
Are One (Ole Ola)’.
Post a Comment