
Wahalifu kila siku wanakuja na mbinu mpya ambapo Polisi nchini Canada
wanamsaka mtu hatari mwenye silaha ambaye amevaa mavazi kama ya
muigizaji wa filamu za mapigano Rambo. Mtu huyo amewaua kwa kuwapiga
risasi maafisa watatu wa polisi na kujeruhi wengine wawili katika tukio
hilo la pamoja.
Mashambulizi hayo ya risasi yamefanyika wakati polisi walilipokea
simu juu ya mtu aliyekuwa na silaha Kaskazini mwa mji wa Moncton katika
Jimbo la Pwani ya Mashariki ya New Brunswick.
Post a Comment