
Hukumu hiyo ilitolewa jana na
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe, Faustine Kishenyi.
Hakimu Kishenyi alisema mahakama imeridhika mshitakiwa hana hatia baada ya
upande wa mashitaka
kushindwa kuthibitisha kosa
lake.
Alisema mbali ya Polisi kushindwa kuwasilisha vielelezo mahakamani kama
ilivyo katika hati ya mashitaka,
pia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka unaonekana kuzingatia
zaidi maslahi yake; hivyo
haujitoshelezi kumtia mshitakiwa hatiani.
Kwa mujibu wa hakimu, upande wa
mashitaka umeshindwa kuwasilisha
CD iliyochukuliwa wakati mshitakiwa akitenda kosa huku polisi watatu wakiwa ndio pekee wametoa
ushahidi dhidi ya mshitakiwa.
Amesema ushahidi uliothibitishwa na shahidi
kutoka nje ya jeshi hilo ambalo
ndio linadai kulengwa, unaonekana kuwa
na maslahi ya upande mmoja hivyo hauwezi kutumika kumtia hatiani mshitakiwa.
Awali ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa
Polisi, Samwel Onyango kuwa
Machemli (39) alitenda kosa la
uchochezi Oktoba 23 mwaka 2011 wakati
anahutubia mkutano wa hadhara katika
Kijiji cha Nyamanga kisiwani Ukara.
Ilidaiwa Machemli kwa makusudi alichochea wananchi
wazuie shughuli za polisi na
hata kuwashambulia wakienda katika
maeneo yao kutafuta wahalifu.
إرسال تعليق