
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk, Richard Sezibera ameasa
wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EALA) kuacha tabia ya
kudhalilisha Baraza la Mawaziri.
Amesema baraza hilo ndicho chombo kinachotoa ushauri kwa wakuu wa nchi wanachama kuhusu masuala ya jumuiya hiyo.
Aidha ametoa rai kwa wabunge wa
bunge hilo kuacha kudhalilisha Bunge na jumuiya
kwa kulifanya kuwa sehemu ya migogoro isiyoisha.
Ametaka waache tabia ya kudharau utendaji kazi katika ofisi mbalimbali
zilizopo ndani ya jumuiya hiyo.
Sezibera aliyasema hayo jana
ndani ya Bunge wakati alipokuwa akitoa hoja wakati wa kujadiliwa na
hatimaye kupitishwa kwa bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo
imepita bila kupingwa.
Alisema si busara kwa wabunge wa EALA kudhalilisha Baraza la Mawaziri
ambao ndio wanaowashauri wakuu wa nchi na kuongeza kuwa ni vyema wabunge hao
wakahakikisha wanasimamia masuala yanayohusu nchi wanachama wa jumuiya hizo.
Waziri wa EAC kutoka Uganda, Shem Bagaine alisema wanatafuta vyanzo vya fedha vitakavyokidhi
bajeti ya jumuiya hiyo.
Alisisitiza, Agosti m waka huu
watapeleka suala hilo kwenye Kikao cha
Baraza la Mawaziri kujadili mapendekezo ya kukata asilimia moja ya kodi zote za bidhaa za nchi za EAC na ombi hilo likipitishwa
litaweza kupunguza utegemezi wa bajeti
kwa nchi wahisani. Bajeti iliyopitishwa na Bunge hilo ni dola za
Marekani 124,169,625 .
إرسال تعليق