
Shule ya Sekondari ya Lumala ina upungufu mkubwa wa Walimu wa masomo ya Sayansi.
Shule hiyo ina walimu wawili tu wa masomo hayo kati ya walimu 52 waliyopo katika shule hiyo.
Hayo yamefahamika baada ya Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete baada ya
kufanya ziara ya siku moja katika shule hiyo na kupata taarifa kutoka
kwa Mkuu wa shule Bwana Christopher Mafuru.
Mwalimu Mkuu huyo alisema
kwamba,pamoja na ukosefu wa walimu wa masomo ya Sayansi, shule hiyo ina
mradi wa upandaji miti kwa kuzingatia suala zima la utunzaji mazingira
katika maeneo ya shule na makazi.
Shule hiyo ya Lumala imeshaotesha
miche elfu kumi,kati ya hiyo miche 1,000 ni miche ya miti ya kivuli na
maua.Mradi huo ni endelevu na utaendelea kupanda na kuotesha miti kadiri
ya mahitaji ya shule.
Alisema kwamba mradi unakabiliwa
na tatizo la ukame kutokananaukosefu wa mvuahali ambayo imefanya mradi
huo kusimamisha kuotesha miti au miche katika mradi huo. Pamoja na
changamoto hizo,shule ina mpango wa kuotesha miti zaidi ya 40,000 kwa
mwaka 2014/2015.
Na Ofisi ya Makamu wa Rais.
إرسال تعليق