
Waziri
Mkuu, izengo Pinda akifungua Mkutano wa Majadiliano wa Kutangaza Mradi
wa Mabasi yaendayo haraka (Dar Rapid Transit) kwenye ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar es salaam, Juni 3, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)

Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa
Majadiliano wa Kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwenye ukumbi
wa Mlimani City jijiniDar es salaam Juni 3, 2014. Kulia kwake ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa
Ghasia(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu,, Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Dunia nchini, Bw. Philippe Dongier baada ya kufungua Mkutano
waMajadiliano wa kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwenye
ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam Juni 3, 3014. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Mizengo
Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia nasekta binafsi katika mradi
mkubwa wa usafirishaji abiria.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumanne, Juni 3, 2014) wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano yenye
lengo la kuutangaza mradi wa mabasi yaendayo kasi kwenye ukumbi wa
Mlimani City. Mkutano huo wa siku mbili, utamalizika kesho (Jumatano,
Juni 4, 2014).
Waziri Mkuu amesema kutèkelezwa
kwa mradi huo kutatoa fursa za ubunifu utakaowezesha kupatikana kwa
suluhisho la usafiri mijini na hasa kwenye miji inakua kwa kasi barani
Afrika.
”Mbali ya kutoa huduma za hali ya
juu, za haraka na ambazo siyo ghali kwa wakazi wa Jiji la Dar es
Salaam, nia ya Serikali ni kuona mfumo mpya wa matumizi ya kadi kwenye
mpango huu wa usafiri unatumika ipasavyo,” alisema.
Alisema ni matumaini ya Serikali
kwamba wadau kutoka sekta binafsi ambao ni wazawa na wa kutoka nje ya
nchi watashiriki kwenye mradi huu ili uweze kuboresha matumizi ya kadi
ambayo mtu hatatakiwa kulipia fedha taslimu akiwa ndani ya basi bali
kutumia kadi anayoilipia kabla ya kuingia ndani ya basi husika.
Akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali
iliamua kuanzisha mradi huo ili kupunguza msongamano wa magari kwenye
barabara za Jiji la Dar es Salaam.
“Hii ni awamu ya kwanza ambayo
inakaribia kukamilika na inaanzia Kimara hadi Kivukoni na itakuwa na
matawi mawili ya Morocco na Karikoo. Mradi wote una awamu sita za ujenzi
kuelekea maeneo tofauti ya Jiji,” alisema.
Mbali na mradi huo wa mabasi
yaendayo kasi, Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia usafiri wa
majini kwa kutumia boti kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo kama njia
mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
“Vilevile tutaimarisha usafiri wa
reli kama njia nyingie ya kupunguza tatizo hili. Dk. Mwakyembe (Waziri
wa Uchukuzi) ameanza na sote tumeona ni jambo linalowezekana. Cha msingi
ni kuimarisha tu usafiri huu,” aliongeza Waziri Mkuu.
Mapema, akiwakaribisha wajumbe wa
mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bibi Hawa
Ghasia alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo
unafanikiwa.
Pia alitumia fursa hiyo kuishukuru
Benki ya Dunia ambayo alisema imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni
200 kwa ajili ya kufadhili mradi huo.
kutano huo unawashirikisha wadau
mbalimbali wakiwemo wa ndani na wa nje wanaotarajiwa kutoa huduma za
mabasi makubwa na madogo, utoaji tiketi, ulinzi, usafi na huduma za
maduka.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMANNE, JUNI 3, 2014.
إرسال تعليق