Wakati ulimwengu ukiwa katika majonzi baada ya kuripotiwa kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia, habari kutoka Uganda zinaeleza kuwa ndege iliyokuwa imebeba wanajeshi wa Marekani ililazimika kutua kwa dharura barabarani.
Msemaji wa jeshi la polisi la Uganda, Phillip Mukasa amesema ndege
hiyo ndogo ilikuwa imebeba watu nane ikiwa ni pamoja na wafanyakazi
wawili na ililazimika kutua kwa dharura katika mji wa Mityana, kilometa
67 kutoka Kampala.
Ameeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa imekaribia Sudan Kusini lakini
kutokana na kupungukiwa mafuta rubani aliamua kurudi Uganda katika
uwanja wa ndege wa Entebbe.
Hakuna mtu aliyeumia katika tukio hilo na ndege hiyo haikupata uharibifu mkubwa.
إرسال تعليق