Jopo
la mahakimu watatu, lilitoa uamuzi huo jana baada ya kukubali ombi la
Wakili wa Utetezi, Majura Magafu aliyeiomba mahakama kuhamia katika
hospitali hiyo, kwa kuwa mshitakiwa huyo amelazwa.
Maranda na wenzake wanadaiwa kuiba fedha hizo kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia BoT.
Akiwasilisha ombi
hilo juzi, Wakili Magafu alidai kuwa Maranda amelazwa katika hospitali
hiyo na ana tatizo la kukaa, lakini anaweza kutoa ushahidi wake akiwa
amelala. Pia, aliomba mahakama itoe taarifa katika hospitali hiyo ili
waandae utaratibu.
Jopo hilo likiongozwa na Hakimu Mkazi, John Utamwa
lilisema Agosti 11 mwaka huu mahakama itahamia katika hospitali hiyo
kwa ajili ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa huyo na Agosti 12 na 13,
wataendelea kusikiliza kesi mahakamani.
Mbali na Maranda, washitakiwa
wengine ni Farijala Hussein, Ester Komu, Bosco Kimera na Imani
Mwakosya. Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka ya kuwasilisha
nyaraka za uongo, kughushi na kuiba Sh milioni 207 kutoka BoT.
Inadaiwa
kuwa washitakiwa walighushi nyaraka, ambazo ni pamoja na hati za
makubaliano ya kuhamishiwa deni kutoka Kampuni ya General Marketing ya
India kwenda Kampuni ya Rashaz (T) ya Tanzania, ambazo walizitumia kuiba
fedha hizo.
Katika hatua nyingine kesi ya wizi ya Sh bilioni sita za Benki
Kuu
(BoT) kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) inayomkabili Johnson
Lukaza na ndugu yake Mwesiga Lukaza inatarajia kuendelea kusikilizwa leo
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Jana kesi hiyo ilitajwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Hata hivyo, Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe aliahirisha kwa kuwa jopo la mahakimu wanaosikiliza, halikukamilika.
إرسال تعليق