Kenyan Actress alietakiwa kufanya ’12 Years Of Slave’ badala ya ‘Lupita Nyong’o’ ndani ya ‘GOING BONGO’ || BUY On iTUNE NOW

20140709-224808-82088002.jpg
Kenyan actress, Singer na Model ‘Nyokabi Gethaiga’ a.k.a ‘Kabi Gethaiga’ ambae yupo ndani ya ‘East African’ film ‘Going Bongo’ ambayo ipo tayari kununuliwa rasmi kwenye iTune LEO. Film hiyo ambayo imefanywa na mtanzania ambayo ni ya kwanza iliyopo kwenye Level za kimataifa iliyohusisha actors na producers toka Tanzania na Kenya.
20140709-225141-82301298.jpg
Going BONGO’ ni Film ambayo inamzungumzia American doctor ambae ameanza career yake ya udaktari mjini California United States of America, kwa bahati mbaya anajitolea kwenda kufanya kazi ya udaktari nchini Tanzania kwa muda wa mwezi mmoja bila kujua mazingira ya kazi ya nchini humo. Katika story hii, daktari huyo baada ya kukumbana na ugumu wa ufanyaji kazi katika nchi za afrika, baadae aliweza kuelewa na kuzoea mazingira na kujifunza mambo mengi sana katika mila na desturi na kuweza kufanya kazi vizuri kuliko alivyotegemea kutokana na watu wanavyoishi na kushirikisha maisha yao ya kawaida na kazi ambapo aliweza kujenga undugu na urafiki zaidi na wagonjwa katika jamii hiyo.
20140709-225239-82359909.jpg
Film hii ambayo imefanyika jijini Dar Es Salaam Tanzania na Los Angeles California imeleta changamoto kubwa sana katika utengenezaji wa Filamu nchini Tanzania na East Africa kwa ujumla.
‘Nyokabi’ ambae ni actress tokea jijini Nairobi nchini Kenya ambae ameshatokea kwenye production kubwa nchini kenya kama katika filamu ya ‘Half-Life – 2012′ na nyingine iliyofanyika jijini London ijulikanayo kama ‘I Am Slave – 2010′. Inasemekana kuwa alikuwa miongoni mwa actress ambao walifikiriwa kwenye Hollywood Film ’12 Years A Slave’ ambayo nafasi hiyo alifanikiwa kuipata mwanadada ‘Lupita Nyong’o’ ambae amejikusanyia umaarufu mkubwa sana na kujinyakulia Awards za kutosha kuanzia ‘Oscars’ na juzi kuongeza nyingine ya ‘BET Awards’ kwenye role ya ‘Best Actress’. Mpaka sasa msanii Lupita amepata ofa lukuki za filamu huyo Hollywood kutokana na umaarufu alioupata kwenye filamu ya hiyo.


Post a Comment

أحدث أقدم