washiriki katika mkutano wa Wafanyakazi wa Mamlaka
ya vitambulisho vya taifa NIda wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni
rasmi mkuu wa wilaya ya arumeru Munasa Nyirembe leo nje ya jengo la
hotel ya Snowcrest sehemu ambayo mkutano ulikuwa unafanyika
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) , Dickson Maimu akiwa
anaongea na waadhishi wa habari kuhusiana na zoezi lima la ugawaji wa
kitambulisho cha taifa .
washiriki wa mkutano huo wakiwa wanasikiliza kwa makini mkuu wa wilaya wakati akiongea katika ufunguzi wa mkutano huo
======== ====== ==========
Na Woinde Shizza,Arusha.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) , Dickson Maimu amesema
kuwa zoezi la usajili wa watu na kuwapatia vitambulisho hivyo litaanza
katika mikoa ya Lindi,Mtwara na Pwani hivi karibuni hivyo amewataka
wananchi kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo.
Aidha
Mkurugenzi huyo amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo katika
mikoa ya Dar es Salaam na mikoa yote mitano ya Zanzibar sasa wanaelekea
katika mikoa hiyo .
Akizungumza
katika mkutano wa Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo unaoendelea jijini hapa
alisema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia Watanzania kukopesheka kwa
urahisi baada ya kutambulika hivyo kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na
taifa kwa Ujumla,pia kuwatambua wageni na wakimbizi.
Maimu
amesema kuwa serikali imetenga fedha za kutosha katika bajeti kiasi cha
shilingi bilioni 200 ambazo zitasaidia kufanikisha zoezi hilo na
kulikamilisha,tunatarajia baada ya mikoa hiyo itafuata
Kilimanjaro,Arusha na Tanga.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha ,Nyirembe Munasa alisema kuwa
licha ya vitambulisho hivyo kuwasaidia wananchi kiuchumi vitawasaidia
katika masuala ya ulinzi na usalama ,kutatusaidia kuwatambua wachafuzi
wa amani inawezekana wanatoka nje pia kudhibiti ugaidi.
Nyirembe
ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa inatoa elimu ya kutosha kwa
wananchi kwa kupitia vyombo vya habari na taasisi mbali mbali zikiwemo
shule na vyuo ili watanzania wajue umuhimu wa vitambulisho hivyo .
Naye
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo kwa upande wa Zanzibar,Vuai Suleman alisema
kuwa tayari zoezi hilo limekamilika katika nchi hiyo yenye mikoa 5 na
wilaya 10.amewataka watanzania kutoa ushirikiano na kuwa na taarifa
muhimu ikiwemo kitambulisho cha mkazi,cheti cha kuzaliwa,vyeti vya
kukupigia kura ili kufanikisha zoezi hilo la kitaifa.
إرسال تعليق