Kikosi
cha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika Ufukwe wa
Coco Beach chini ya kocha mkuu mpya mbrazil Marcio Maximo tayari kwa
mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015 na mashindano ya
Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Young Africans imeanza rasmi maandalizi ya msimu mpya chini ya kocha
mpya Maximo ambaye alijijengea heshima kubwa miaka minne iliyopita
wakati alipokuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars)
kutokana na falsafa yake ya soka la vijana na kusimamia nidhamu.
Jumla
ya wachezaji 14 kutoka timu ya wakubwa wamehudhuria mazoezi ambapo leo
kikubwa walikua wakifanya mazoezi ya kusaka pumzi, kujenga mwili huku
baadhi ya washabiki wakijitokeza kushuhudia mazoezi ya mbrazil huyo.
Wachezaji waliofanya mazoezi leo ni:
1.Ally
Mustafa "Barthez" 2.Juma Abdul, 3.Swaleh Abdallah, 4.Rajab Zahir, 5.
Mbuyu Twite, 6.Salum Telela, 7.Omega Seme, 8.Hassan Dilunga, 9.Said
Bahanuzi, 10. Andrey Coutinho, 11.Hussein Javu, 12.Juma Kaseja, 13.Nizar
Khalfani, 14.Jerson Tegete
Katika mazoezi ya leo kocha Maximo
ameendelea kuwakosa wachezaji 11 ambao wapo katika timu za Taifa mbali
mbali wakijiandaa na michezo itakayowakabili mwishoni mwa mwezi huu,
wakipigania kucheza fainali za Mataifa Afrika.
Wachezaji walio
kwenye timu ya Taifa Tanzania ni 1.Deo Munish "Dida", 2.Oscar Joshua,
3.Kelvin Yondani, 4.Nadir Haroub "Cannavaro", 5.Saimon Msuva, 6.Mrisho
Ngasa, 7.Pato Ngonyani, 8. Said Juma huku Uganda ikiwa na Emmanuel Okwi,
na Hamis Kizza na Rwanda Haruna Niyonzima.
Mara baada ya mazoezi
ya asubuhi, timu itaendelea na mazoezi tena leo jioni katika Uwanja wa
Bandari - Tandika majira ya saa 10:00 jioni
إرسال تعليق