Jamani Hii si Hatari kweli.

 Ndugu zangu hawa watu wa shirika la Umeme wako wapi inafikia waya wa umeme kupita juu ya paa la nyumba na kuwekewa tambara kuzuiya kuchunika, hii ni hatari kwa wananchi wanaokaa katika nyumba hii huko kinuni siku waya huo ukiwa tayari umeshachunika na kuleta madhara kwa wananchi wa nyumba hii nani wa kulaumiwa ? ZECO au Mwananchi huyu . jioneeni wenyewe na kutowa maamuzi ya jambo hili kazi kwenu wahusika. Kadhia hii imeiona wakati nikiwa katika tembea yangu kinuni leo asubuhi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post