Kundi lililo na uhusiano na mtandao
wa Al-Qaeda nchini Syria Al- Nusra Front limepinga mashambulizi ya
angani yanayotekelezwa na muungano unaoongozwa na Marekani kama vita
dhidi ya Uislamu na kusema kuwa nchi za magharibi na zile za kiarabu
zinazohusika zitalengwa na makundi ya Jihad kote duniani.
Matamshi
hayo yanatolewa baada ya Marekani kusema kuwa ushirikiano na washirika
wake wa kiarabu umefanya mashambulizi zaidi dhidi ya wanamgambo wa
Islamic State nchini Syria na Iraq.
Wizara ya ulinzi nchini
Marekani ilisema kuwa ndege za kijeshi zilishambulia mji wa Raqqa nchini
Syria ambao ni ngome ya wanamgambo pamoja na maeneo yanayodhibitiwa na
kundi la Islamic state karibu na mji wa Kikurdi wa Kobane karibu na
mpaka na Uturuki.
إرسال تعليق