TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PIGA KITABU NA LAPF”
WANACHAMA WA LAPF KUNUFAIKA NA FAO LA ELIMU
Bilioni 3 kutumika mwaka wa masomo 2014 – 2015 kutoka mfuko wa pensheni wa LAPF kwa wanachama wake.
15 Septemba 2014, Dodoma:
Wanachama wa mfuko wa penseni wa LAPF kunufaika na fao jipya
lilozinduliwa hivi karibuni nchini kwa Baraka zake Waziri wa nchi ofisi
ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia. Fao hilo lijulikanalo kama
‘Piga Kitabu na LAPF’ limelenga kuwakopesha wanachama wa LAPF mikopo ya
elimu ya juu kwani ni ombi la muda mrefu kutoka kwa wanachama wa mfuko
huo. Hivyo kwa kuthamini na kuona umuhimu wa elimu Mfuko wa Penseni wa
LAPF umjibu kiu yao ya muda mrefu ili kumpunguzia mzigo mwajiri.
Akiongea kutoka Dodoma,
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bwana Eliud Sanga alieleza kuwa mfuko wa
Pensheni wa LAPF una huduma nyingi na ambazo zimelengwa kwa ajili ya
jamii na hususani zinazochangia sana kwenye maendeleo. “Huduma hii mpya
ya Fao la Elimu imetengewa shilingi Bilioni Tatu (3) kwa mwaka huu wa
fedha ikiwa ni kianzio cha mfuko huu, tunaahidi mwaka unaofuata fao hili
litatengewa bajeti kubwa zaidi kutokana na umuhimu wake katika nchi
yetu, wanachama wengi wameshanufaika mpaka sasa na wengine wengi zaidi
wanazidi kutuma maombi ya kupata mkopo wa elimu ya juu. Fao hili
litawanufaisha wanachama maelfu na maelfu, wanachama wengi watume maombi
kunufaika na huduma hii”
“Mwanachama anatakiwa kujaza fomu
ya mkopo wa elimu LAPF/LON.2, ambayo hupatikana katika ofisi zote za
LAPF pamoja na ofisi za waajiri wachangiaji na pia kwenye tovuti ya LAPF
www.lapf.or.tz. Baada ya
kukamilisha fomu na kuambatisha vielelezo vinavyotakiwa atawasilisha
fomu hiyo kwenye ofisi za LAPF au atatuma kwa njia ya posta. Fao hili la
Mkopo wa Elimu kwa mwanachama utalipwa moja kwa moja chuoni kila mwaka
wa masomo kwa taratibu za chuo husika na urejeshaji wake utakuwa kwa
muda wa miaka mitano tangu ulipoanza kutolewa” Aliongeza Bwana Sanga.
‘Piga Kitabu na LAPF’ ni fao la
elimu litakalotolewa kwa mwanachama yoyote wa lapf ambaye amekidhi
vigezo kama kupata kibali cha kusoma toka kwa mwajiri wake, barua
(admission letter) ya kukubalika kujiunga na chuo cha hapa nchini
kilichosajiliwa na nacte au tcu na awa na michango inayozidi kiasi cha
mkopo unachoombwa kwa asilimia 25.

Post a Comment