Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
Ripoti
zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo
walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wadadisi
wanasema kuwa mauaji hayo ini ishara ya ushawishi wa kundi la Al
shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na
vikosi vya muungano wa Afrika.
Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.
Post a Comment