Professor Jay amesema baada ya kuwekeza pesa nyingi kwenye kazi
zake mpya ‘Kipi Sijasikia’ na ‘Tatu Chafu’ ameamua kupandisha gharama ya
show zake huku akiwataka mapromota wa Tanzania kutoogopa kwakuwa
hawatashindwana.
Professor amesema ameamua kupandisha gharama ili kufidia uwekezaji alioufanya kwenye video mbili za nyimbo zake mpya.
“Unapozidi kuinvest kwenye muziki wako lazima na matunda yako
yaongozeke kidogo. Hata gharama za show kwa sasa hivi vipo juu kwasababu
ya kufidia na kuweza kutengeneza kazi zaidi ili kuendelea pale
nilipochia.” Professor ameiambia Bongo5.
“Kwahiyo kwa hizi nilizofanya sasa hivi ili niweze kufanya kubwa
zaidi ni lazima hii hela yangu irudi na iongezeke, lazima dau liongezeke
kuliko kufanya kazi nyingi kwa dau dogo. Ni heri ufanye kazi chache kwa
dau zuri. Sipendi kuwa muongo kama watoto wengine kwenye gharama ya
show zangu lakini sio gharama ndogo na kubwa kwa mapromota kwahiyo
wasiogope kum-face Professor Jay.”
“Promoter wengi wanajua madau yetu ni makubwa wanaanza kuogopa
kum-face Professor kwaajili ya dau lake kubwa. Hii ni time ambayo
umefanya kazi nzuri mashabiki wako mpaka wa kijijini wanakuhitaji sasa
ukiweka dau kubwa utawafikia vipi? Mimi naamini nipo Professor Jay kwa
miaka mingi kwaajili ya mashabiki wangu wa mjini na vijijini, ikiwa nje
ya nchi hilo ni suala lingine kwa sababu tunakuwa tuna deal na watu
wengine international hata kuchaji tunachaji cha dola. Lakini tukiwa
hapa hapa nyumbani kusema kweli hatuwezi kushindwana na mapromota wa
ndani yaani hapa nyumbani,” alisema Professor Jay.
Pia Professor amezungumzia matunda ya mapema aliyoyapata baada ya
kuwekeza pesa nyingi kwenye video za Kipi Sijasikia na Tatu Chafu.
“Kusema kweli sasa hivi nimekuwa booked sana, hapa ninapoongea na
wewe ninashow Nairobi, ninashow KampaLa na nina show Kongo. Pia kwa
sababu watu wamekuwa interested sana na kazi zangu mpya, kwa muda mfupi
nimeshafika sehemu na watu wameshaanza kunifanyia booking. Achana na
makampuni ya hapa nchini kuna makampuni ya simu wanataka kufanya kazi na
mimi, nadhani huu mwezi unaofuata utakuwa busy sana. Kwa sasa hivi
nimeacha kuchukua show kwa sababu kipindi hiki cha mwanzo bado nipo
kwenye promotion ya huu wimbo na hizi video.”
إرسال تعليق