Mamia
ya waandamanaj wa Hong Kong wamezingirwa na Askari polisi wanaowataka
kusitisha maandamano na mkusanyiko wao karibu na ofisi za Makao makuu ya
serikali.
Waratibu wa maandamano hayo wamekaidi amri hiyo na
kuwataka watu wengine zaidi kujitokeza ili kuwaunga mkono katika madai
yao ya kuitaka China iwaachie uhuru wa kumchagua kiongozi wao katika
uchaguzi ujao wa mwaka 2017.
Kiongozi wa Mamlaka ya Hong Kong C Y
Leung amesema serikali yake imesikiliza na kuzingatia madai ya
waandamani lakini inapingana na mpango wao wa kujitenga.
‘’Mimi
na serikali yangu tutazingatia sheria za msingi na uamuzi unaostahili wa
NPCSC,tutajaribu juhudi zote kutekeleza uchaguzi wa kiongozi mkuu kwa
kila anayestahili kupiga kura atafanya hivyo mwaka 2017. Serikali
itaanzisha hatua inayofuata ya majadiliano kuboresha katiba hivi hivi
karibuni. Inasihi sekta mbalimbali za jamii kushiriki katika majadiliano
yenye mantiki kwa Amani na kwa kufuata sheria, kufikia makubaliano na
kukubali tofauti pamoja na kuruhusu watu milion tano wenye uhalali wa
kupiga kura hapa Hong Kong kumchagua kiongozi mkuu mwaka 2017 mtu mmoja
kura moja’' amesema Leung Chung-ying.
‘mimi na serikali yangu
tumekuwa wasikivu kwa raia na tumejitolea kudumisha jamii yote. Wananchi
wanatakiwa kutoa wanayoyahitaji kwa Amani, mantiki na kisheria, na
kuheshimu na kuzingatia mitazamo mbalimbali katika jamii. Serikali ya
SAR ya Hongkong imeazimia kupinga utawala usio wa kisheria wa ofisi za
serikali kuu au makao makuu ya wilaya ‘utawala wa seriakli kuu’’. Polisi
wanajitambua kukabiliana na hali kwa wakati kwakuzingatia sheria’’
Ameongeza
إرسال تعليق