MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Togo, Emmanuel Adebayor yuko safarini kwenda Kampala tayari kwa mechi ya
wiki hii ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika, Afcon 2015
dhidi ya Uganda The Cranes.
Siku chache zilizopita Adebayor
hukuwepo kwenye kikosi cha Togo wakati wa mazoezi mjini Lome na hali hii
ilizua wasiwasi kwamba angekosa mechi hiyo muhimu.
Hata hivyo, Supersport.com
imethibitisha kuwa nyota huyo anayekipiga klabu ya Tottenham
inayoshiriki ligi kuu soka nchini England amekuwepo Uganda asubuhi ya
leo akitokea Nairobi.
Togo haina pointi yoyote kufuatia kupigwa 2-1 na Guinea mjini Casablanca na 3-2 kutoka kwa Ghana katika uwanja wao wa nyumbani.
Mechi dhidi ya Uganda ndio
itatoa picha halisi ya nani ana nafasi kubwa ya kufuzu katika mashindano
hayo yakayofanyika nchini Morocoo.
إرسال تعليق