AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KUTOKANA NA TUHUMA ZA KUVUNJA NYUMBA NA KUIBA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 10.10.2014.
  • MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KUTOKANA NA TUHUMA ZA KUVUNJA NYUMBA NA KUIBA.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SITA AKIWEMO MGANGA WA KIENYEJI KWA TUHUMA ZA KUPIGA RAMLI CHANGANISHI.
  • MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA TETE WILAYA YA CHUNYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA JUMA, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30 ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKANA NA TUHUMA ZA KUVUNJA NYUMBA YA JAPHET SANGA (31) MKAZI WA KITONGOJI CHA CHAPAKAZI – MBALIZI NA KUIBA TV, KING’AMUZI NA DECK VYOTE VIKIWA NA THAMANI YA TSHS. 350,000/=.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 03:00 HUKO MAENEO YA MLIMA RELI – MBALIZI, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MAREHEMU USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:45 ALIVAMIA NYUMBANI KWA JAPHET SANGA NA KISHA KUVUNJA MLANGO WA NYUMBA HIYO NA KUIBA VITU HIVYO NA NDIPO JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZILIFANYWA NA HATIMAYE KUKAMATWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOANZA KUMPIGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI – MBALIZI KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA, ANATOA RAI KWA WANANCHI KUJENGA TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAWEZE KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
 KATIKA TUKIO LA PILI:
 MGANGA WA KIENYEJI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MUSSA SIWELU (27) MKAZI WA MBALIZI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUPIGA RAMLI NA KUSABABISHA TISHIO LA MAUAJI KATIKA TARAFA YA MSANGANO, WILAYA YA MOMBA.
 MGANGA HUYO ALIKAMATWA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 03:00 HUKO KATIKA KIJIJI CHA NTUNGWA, KATA YA CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
 AIDHA, KATIKA TUKIO HILO WATU WATANO AMBAO WANADAIWA KUMLETA MGANGA HUYO KIJIJI HAPO PIA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1. FRANK SILUNGWE (28) 2. JUMA JIPSON (35) 3. LOTO JULIUS (16) 4. GERVAS JIPSON (44) NA 5. LOCK MARKO (26), KYUSA WOTE WAKAZI WA NTUNGWA.
 TAARIFA ZA MISAKO:
 MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA TETE AITWAYE YUSTA CREDO (36) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 05.
 MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 09.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA TETE, KATA YA KANGA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA. 
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Post a Comment

أحدث أقدم