
Wananchi wa Tunisia leo wamemfukuza Balozi wa Marekani katika kituo kimoja cha kupigia kura kwenye uchaguzi wa bunge uliofanyika leo Jumapili nchini humo.
Wapiga kura huko Tunisia walipiga nara na kulaani uingiliaji wa Marekani
na Qatar katika masuala ya ndani ya nchini mwao na hivyo kumfukuza
Balozi wa Marekani aliyekuwa anatembelea kituo kimoja cha kupigia kura
huko Tunis mji mkuu wa Tunisia.
Vyama, makundi na mirengo mbalimbali ya kiraia, vyama na shakhsia huru wa kisiasa wa
Tunisia viliwataka wananchi wa nchi hiyo kushiriki kwa dhati na kwa
wingi katika uchaguzi wa leo wa bunge ili kufungua ukurasa mpya wa
maisha ya wananchi na serikali nchini humo.
Weledi wa mambo wanaamini kuwa, kufanyika uchaguzi wa leo wa bunge huko
Tunisia na kutangazwa matokeo yake kutahitimisha kipindi kilichojaa
mivutano na hivyo nchi hiyo itakuwa imeingia katika kipindi kipya cha
harakati za kisiasa na ujenzi mpya.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
إرسال تعليق