Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara
Ni
miezi sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram
kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa
Nigeria, wasichana watatu ambao wametoroka wamezungumza katika mahojiano
maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC.
Tukio hili linakuja wakati
serikali ya Nigeria ikiwa katika makubaliano ya kusimamisha mapigano
dhidi ya Boko Haram hatua itakayo saidia kuwaachilia huru wasichana
waliotekwa na kundi hilo .
'' nilikuwa nataka kurukia nje wakati
msichana mwenzangu aliponikamata kwa nyuma na kusema watakupiga risasi
kama utafanya hivyo. Nikasema, nini utofauti wataniua mimi hapa na
kuacha maiti yangu ikusachukuliwa nilikuwa nalia na kuomba mpaka
tulipoifikia kambini" Anasimulia msichana mmoja alitoroka mikononi mwa
Boko Haram
Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa
ya BBC, Msichana huyu anakumbuka jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati
wanapinaji wa Boko Haramu walipomteka yeye na wasichana wengine.
Zaidi
ya wasichana 200 kati miongoni mwao walikuwa walitekwa lakini wale
waliokimbia walibahatika kutoingia katika hofu kubwa kwenye mikono ya
watekaji.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam la
Human Rights Watch limesema wanawake wanaoshikiliwa na kundi la Boko
Haramu wamekuwa wakinyanyaswa, kubakwa na hata kulazimishwa kuolewa.
Katika
ripoti mpya ya shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa Kiislam
wamewawateka wanawake Zaidi ya 500 na wasichana tangu mwaka 2009.
Serikali
ya Nigeria hivi karibuni imetangaza makubaliano ya kusimamisha mapigano
dhidi ya Boko Haram ambayo hatua itakayawafanya wanamgambo ho kuachilia
huru wasichana wa hao waliotekwa huko Chibok.
Lakini Boko Haram
wenyewe hawajawahi kuthibitisha makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano
na hakuna dalili zozote za kuachiwa kwa wasichana haohivi karibuni.
Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia bado yanawasumbua.
إرسال تعليق