Bibi
Harusi Mariam Juma akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa kigoma Maweni
baada ya kunusurika kwenye ajali ya boti ambayo iligonga mwamba na kuzama
kwenye ziwa Tanganyika.
WATU
watatu wamekufa na wengine zaidi ya 20 wameokolewa wakiwemo bwana na bibi
harusi ambao walitoka kufunga ndoa kufuatia boti waliyokuwa wakisafiria kugonga
mwamba na kuzama ndani ya ziwa Tanganyika.
Kamanda
wa polisi mkoa Kigoma, Jafari Mohamed amesema tukio hilo la jana liemtokea katika
kijiji cha Kalalangabo wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.
Kamanda
Mohamed amesema idadi ya watu haijulikani kwa kuwa mtumbwi ulisafiri nje ya
taratibu za kawaida ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya usalama wa nchi kavu na
majini (SUMATRA).
Kamanda
huyo wa polisi alisema kuwa vikosi vya jeshi la wananchi wa Tanzania kwa
kushirikiana na wavuvi waliowahi kufika katika eneo hilo walifanikiwa kuokoa
watu 20 ambao walikimbizwa hospitali ya mkoa kigoma Maweni kwa matibabu na
wengine inawezekana walikimbia ili kupoteza ushahidi wa idadi ya abiria
waliokuwa kwenye boti hiyo.
Kwa
upande wake Mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa kigoma Maweni, Haika Masula
amethibitisha kupokelewa kwa miili mitatu ya watu waliofariki kwenye tukio
ambapo mmoja ametambuliwa kwa jina la Salama Juakali huku maiti mbili za watoto
zikiwa hazijatambuliwa hadi sasa.
Naye
Kaimu Mwenyekiti wa Wavuvi kwenye Mwalo wa kibirizi mjini Kigoma, Sendwe
Ibrahimu alisema kuwa katika mahojiano na watu mbalimbali waliokuwa kwenye boti
hiyo kumekuwa na takwimu tofauti za idadi kamili ya watu waliopanda boti hiyo
huku wengine wakieleza kuwa ni abiria 80, wengine abiria 70 huku baadhi ya
ndugu wakieleza kuwa jumla ya watu 40 waliondoka nyumbani kwao Mwandiga
kulikofanyika harusi ili kurejea kijijini kwao Mtanga Mwambao wa Kaskazini wa
ziwa Tanganyika.
Ajali
hiyo imetokea wakati Shaban Hussein na Mariam Juma (18) wakazi wa kijiji cha
Mtanga wakitoka kufunga ndoa kwenye kijiji cha Mwandiga Kigoma vijijini
nyumbani kwa bibi harusi.
Bwana
harusi Shaban Hussein aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo leo asubuhi wakati
hali ya bibi harusi iikimarika.
Source:Fadhili,
Habarileo Kigoma
Post a Comment