Mhe, Said Hassan Said |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe,
Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo umeaza
leo 7,Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa
mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984
na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
إرسال تعليق