Mwanamke
aliyebadili jinsia yake ya kiume na kuwa mwanamke na kutaka jina lake
kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani ameshinda kesi yake dhidi ya
baraza la kitaifa la mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha
baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha hali yake
mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia
yake kubadilika kabisa.
Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa
la mitihani nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia
yake kwenye cheti hicho kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke
licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi la serikali.
Jaji
Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la
Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa
mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya
kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye
cheti hicho haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake wala alama
alizopata Audrey na kuondolewa kwake vile vile hakuna athari yoyote.
Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa.
'Audrey ni mwanadamu ambaye anajitambua kwama mwanamke wala sio kama mwanamume jinsia aliyozaliwa nayo,'' alisema jaji.
Jaji
alisema kuwa katiba ya nchi inaamrisha watu kuwaheshimu wengine kama
ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo inahusu mambo mengi
ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa.
Aliongeza kuwa ili Audrey
kuhisi kuwa sawa anapaswa kukubalika kama alivyo na kumyima haki hiyo ya
kubadilisha jina lake katika chati chake itakuwa ukiukwaji wa haki zake
za kibinadamu.
Wakili wa Audrey, aliambia mahakama kuwa mteja wake alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea matibabu.
إرسال تعليق