Kamanda wa Polisi mkoani Iringa (RPC),Ramadhani Mungi
Na Friday Simbaya, Iringa
Mwanafunzi
wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lugalo ameuawa kwa kukatwa
na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiofahamika kisha kupora
pikipiki yake ambayo haijafahamika namba za usajili.
Kamanda
wa Polisi mkoani Iringa (RPC),Ramadhani Mungi amewaambia waandishi wa
habari ofisini kwake leo kuwa Salehe Khamis (18) aliuawa tarehe
06/10/2014 majira ya saa 6:15 usiku katika Kitongoji cha Kikungwe
Igumbilo, Kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa.(Martha Magessa)
RPC alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni pamoja na kuwania mali, ambapo hata hivyo, watuhumiwa wanatafutwa na jeshi la polisi.
Wakati
huohuo, Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mmoja dereva wa lori
aina ya Isuzu kwa kusababisha kifo cha mtembea kwa miguu huko katika
Kijiji cha Itimbo Kata ya Ihimbo, Tarafa ya Kilolo mkoani Iringa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alimtaja marehemu kuwa ni Linus
Mwirafi (45) mkazi Kijiji cha Itimbo kwa kudondokewa na lori hiyo baada
ya kupinduka.
Alisema
kuwa gari hilo lenye namba za usajili T 244 CNK aina ya Isuzu
likiendeshwa na Yoktani Kikula (25) mkazi wa Ipogolo lilipunduka na
kumdondokea mtembea kwa miguu huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.
RPC
alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 05/10/2014 majira
06:00hrs katika kijiji cha Itimbo wilayani Kilolo, mkoani Iringa, na
kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva amekamatwa.
إرسال تعليق