Waandilizi
wa dimba la taifa bora barani Afrika ACN wanasema kuwa hakuna
mabadiliko yoyote ya tarehe ya michuano hiyo licha ya ombi la mwenyeji
wa mechi hizo Morocco la kutaka michuano hiyo kuahirishwa.
Serikali
ya Morrocco imeliandikia shirikisho la soka barani Afrika CAF ikilitaka
kuahirisha mechi hizo kutoka january 17 hadi February 8 kutokana na
mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
CAF imesema kuwa italijadili ombi hilo katika mkutano ujao wa kamati kuu ya shirikisho hilo mnamo Novemba 2.
Baadaye rais wake Issa Hayatou atakutana na maafisa wa Morocco siku itakayofuata.
Zaidi
ya watu 4000 wamepoteza maisha yao kutokana na ugonjwa wa Ebola ambao
ulizuka katika eneo la Afrika Magharibi mwanzoni mwa mwaka huu.
Wizara
ya afya nchini Morocco ilitoa ombi hilo siku ya ijumaa ili kuzuia
matukio ambayo yanahusisha mataifa yalioathirika na ugonjwa wa ebola.
Siku
ya jumamosi CAF ilijibu ombi hilo na kusema kuwa '' Caf imesajili ombi
hilo na inasisitiza kuwa hakuna mabadiliko yoyote yaliofanyika kuhusu
mashindano hayo'',.
Post a Comment