Timu
ya Vijimambo inamasikitiko makubwa ya habari ya upotoshaji iliyoandikwa
na gazeti la Jamhuri lililobeba kichwa cha habari "AUNTY EZEKIEL ATANUA
NA WAZIRI NYALANDU MAREKANI" yakiwemo magazeti mengine yaliyodandia
kuandika habari hii bila kujua ukweli upo wapi. Timu ya Vijimambo
ikiwemo kamati ya maandalizi imechukizwa sana kwa Gazeti hili kuandika
habari ya kizushi na inayojeruhi hisia ya familia ya Mhe. Waziri Lazaro
Nyalandu.
Habari
hii ni uongo ulioandikwa kichochezi na mwandishi anayeitwa Alfred
Lucas. Timu ya Vijimambo haikufurahishwa na uongo huu pamoja
na VIJIMAMBO BLOG kuwa ndio wahusika wakuu, mwandishi alitakiwa
kutupigia simu ili aweze kupata habari ya upande wa pili.
Katika
gazeti hilo pia limeandika "Aunty Ezekiel amekaa Marekani siku 14"
Ndugu mwandishi Aunty Ezekiel amekaa Marekani siku 10 tu amekuja Sept
13, 2014 na ameondoka Sept 24, 2014 na Aunty Ezekiel hakuja kupumzika
huku na Waziri kama ulivyopotosha na uandishi wako wa uchochezi, uliojaa
chuki na husda kama nilivyosema hapo awali kwamba Aunty Ezekiel
ameingia Marekani siku ya Jumamosi Sept 13 na Mhe. Waziri Lazaro
Nayalndu ameingia Marekani siku ya Ijumaa Sept 12, 2014. Aunty Ezekiel
na msanii mwingine wa Bongo Flava Kassim Mganga safari zao zimeratibiwa
na Kamati nzima ya Vijimambo kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Jumuiya ya Watanzania DMV huku
wakiwezeshwa na wadhamini mbalimbali waliojitokeza kudhamini tamasha
hilo la Utalii.
Wenyeji
wa wasanii hawa walikua timu ya Vijimambo pamoja na kamati yake. Lengo
la wasanii hawa kama walivyokuja wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole
ni kuonyesha utamaduni wetu na Utalii kupitia soko la wasanii wa
Tanzania ikiwemo kuwatangaza wasani wetu kimataifa.
Ndugu
mwandishi Aunty Ezekiel na Waziri wameonana mara moja tu usiku wa Sept
13, 2014 kwenye kilele cha sherehe ya Utalii na baada ya hapo hawakuwahi
kuonana tena na baada ya sherehe ya Utalii Jumatatu Mhe. Waziri
Nyalandu alisafiri kuelekea California kuzindua kampuni ya Utalii ya
Tanzania Safari and Tourism inayomilikiwa na Balozi wa Heshima Ahmed
Issa na hakuwahi kurudi tena Washington, DC mpaka siku aliyoondoka.
Ndugu
mwandishi sababu iliyomleta Mhe. Waziri nchini Marekani ni kutokana na
ujumbe wa Utalii na kukemea ujangili na Mhe.. Lazoro Nyalandu ndiye
aliyekuwa mgeni rasmi kama ilivyokua kwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
alipokua mgeni rasmi kwenye tamasha la Utamaduni la Kiswahili.
Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknologia Mhe. January Makamba na mkewe
wakiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles huku wakipokelewa na
Afisa Mindi Kusiga wakati huo akiwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,
kushoto ni Mwenyekiti kamati ya Vijimambo Bw. Baraka Daudi.Mhe.
Janauary Makamba alikua mgeni rasmi wa sherehe ya Uhuru miaka 51.
Tunaiomba
Serikali kuyachukulia hatua zinazositahili magazeti kama haya
yanayoweza kujeruhi hisia ya mtu na habari ya uongo kama hii ni sumu
kubwa kwenye mahusiano na upendo kwa familia na siku zote habari ya
uongo hua na nguvu kuliko ukweli.
Mwisho
timu ya Vijimambo na kamati ya maandalizi tunaomba radhi kwa Mhe.
Waziri Lazaro Nyalandu kwa usumbufu na maumivu ya gazeti la Jamhuri na
magazeti mengine yaliyodandia habari yalivyosababisha kwako na familia
yako. Siku zote tutakua mstari wa mbele kufanyakazi na wewe popote na
wakati wowote.
Aunty Ezekiel akitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York, kulia ni Balozi Tuvako Manongi Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.
Post a Comment