Kipa Mkongwe, Mark Schwarzer (Kushoto) amecheza mechi nne tu tangu awasili Chelsea msimu uliopita
CHELSEA imetupilia mbali ombi la Fulham kutaka kumrejesha kipa mkongwe, Mark Schwarzer katika uwanja wa Craven Cottage.
Kipa
huyo aliwasili Stamford Bridge mwaka 2013 kama kipa wa ziada, lakini
amecheza mechi nne tu Chelsea na amebaki kuwa kipa namba tatu nyuma
ya Thibaut Courtois na Petr Cech.
Fulham imeomba kumchukua kipa huyo mwenye miaka 42 kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu, lakini Jose Mourinho amekataa ofa hiyo.
إرسال تعليق