TIMU
ya Taifa ya Nigeria jana ijumaa ilishindwa kufanya mazoezi katika
uwanja wa Khartoum kujiandaa na mechi dhidi ya Sudan kutokana na uwanja
kujaa maji kufuatia mvua kubwa kunyesha Khartoum, mji mkuu wa Sudan.
Super
Eagles waliwasili mapema jana na walikuwa na ratiba ya kufanya mazoezi
jioni, lakini ikashindikana kutokana na tatizo hilo.
Msemaji wa timu ya Taifa ya Nigeria, Ben Alaiya baadaye alikiri kuwa wanatarajia kuripoti suala hilo CAF.
Sudani
na Nigeria sitachuana leo jumamosi katika mchezo wa makundi kuwania
kufuzu fainali za mataifa ya Africa mwakani nchini Morocco.
إرسال تعليق