Afisa
Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani kushoto Akimkabidhi Msaada wa
Kompyuta Mkuu wa Chuo Kikuu teule cha Marian Father Luke Mbefo ambapo
Kompyuta hizo zitatumika katika Kuhifadhi Nyaraka mbalimbali za Maktaba
Mkuu
wa Chuo Kikuu teule cha Marian Father Luke Mbefo kulia akimshukuru
Afisa Mahusiano wa PSPF Bi. Coleta Mnyamani kwa msaada huo
Mwakirishi
wa Shirika la Roho Mtakatifu Father Nicetas Kyara akitoa neno la
Shukurani Baada ya kukabidhiwa msaada wa Kompyuta Mbili za kisasa kutoka
Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Afisa Mahusiano wa PSPF Bi. Coleta Mnyamani akizungumza neno Baada ya kukabidhi Msaada huo
Afisa
wa Fedha kutoka PSPF Bwana Samwel Haule Akizungumza Jambo wakati wa
Makabidhiano wa Kompyuta hizo katika Chuo Kikuu teule cha Marian
Mkuu
wa Chuo teule cha Marian Father Luke Mbefo wakiteta Jambo na Afisa
Mahusiano wa Pspf Bi Coleta Haule Baada ya Kukabidhi Msaada huo
Picha ya Pamoja ya Viongozi wa PSPF na Chuo Kikuu teule cha Marian
Kulia
ni Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka akimkabidhi Kompyuta 10
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu na
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt. Ally S.
Mcharazo kwa niaba ya chuo hicho
Meneja
wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka akizungumza na wanafunzi wa Chuo
cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu pamoja na wagani waalikwa wakati wa
kukabidhi msaada huo wa kompyuta 10 za kisasa
Rais wa Chuo cha Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu Daudi Joho akitoa neno la Asante Baadhi ya Kukabidhiwa Msaada huo
Mbele ni Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu
wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt. Ally S. Mcharazo akitoa
neno la Shukurani
Baadhi ya wanafunzi wakisoma Vipeperushi vya PSPF
Wanafunzi wakiwa wanafuatilia kwa makini
Kila mtu anachukua Kumbukumbu
Mfuko
wa pensheni wa PSPF waendelea kukuza elimu ya Tehama katika vyuo
mbalimbali hapa nchini kwa kutoa msaada wa jumla ya kompyuta 12 katika
chuo cha Ukutubi Uhifadhi wa Nyaraka Bagamoyo na chuo Teule ambacho
kitakuwa kikiendeshwa chini ya saint augustine's university (SAUTI)
ambapo kompyuta kumi (10) zimetolewa katika
chuo cha Ukutubi Uhifadhi wa Nyaraka na Mbili zimetolewa katika chuo
teule cha cha Mariana university College vyote vilivyopo bagamoyo katika
mkoa wa pwani.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo afisa mahusiano wa PSPF Bi. Coletha
Mnyamani amesema zoezi hilo limeanza lakin halitaishia hapo kwani ni
zoezi endelevu kwani wameamua kusaidia jamii hususani kwa wanafunzi
ilikuweza kuwajengea ujuzi katika masomo yao pamoja na kutunza nyaraka
zao kisasa na sio katika makaratasi kama ilivyo kuwa hapo zamani
Kwaupande
wake Meneja wa Wa PSPF Mkoa wa Pwani Bw.Msafiri S Mugaka amesema kuwa
wameweza kutimiza ahadi waliyo ahidi kwa chuo cha Ukutubi Uhifadhi wa
Nyaraka na kuweza kutoa msaada kwa chuo teule cha Mariana university College Hivyo wawaomba wananchi kuiamini na kuendelea kuwa wanafamilia wa mfuko huo wa pensheni
Naye
Mwenyekiti wa Baraza la chuo cha Ukutubi Uhifadhi wa Nyaraka na
mkurugenzi wa wa Bodi ya Huduma za Maktaba –Tanzania Ally Mcharazo
kilichopo Bagamoyo wakati akipokea msaada huo kutoka kwa maafisa wa
mfuko wa PSPF makao makuu Dar es saalam Amesea wanatoa shukrani kwa
Mfuko huo kwani umeweza kuwasogeza katika huduma za kisasa kwa
kuwapelekea kompyuta hizo nyaraka zote zitakuwa zikitunzwa katika hali
iliyo salama na sio katika hali ya kizamani na kazi kuenda kwa haraka
zaidi kwani kompyuta husaidia katika kuokoa muda kazini.
Pia
Bw.Samweli Haule ambaye ni afisa Wa Fedha Wa Mfuko Wa Pensheni wa PSPF
Aliweza kutoa maneno ya kuwaasa wanafunzi kwa kuwa makini na wao hawata
choka kutoa msaada pindi wanapo kuwa wamekwama ili kuweza kuwaweka
wanafunzi wote katika hali ya kisasa zaidi
Mkuu
wa Chuo cha Mariana university College Father Luke Mbefo pia naye
aliweza kushukuru Mfuko wa PSPF kwa kuona umuhimu wa kuweza kusaidia
upande wa elimu kwa kuchangia kwa aina mbalimbali bila kuchoka na
kuchagua rangi wala dini
Hivyo
Mfuko wa Pensheni PSPF Umetoa wito kwa wananchi pamoja na vyuo
mbalimbali kwakuwa wao wapo kwamoyo kwaajili ya wananchi na kuhakikisha
kuweza kuikomboa elimu yetu kwa kuipelekea wepesi zaidi katika hali ya
udigitali kuachana na analogia,kwani huop ni mwanzo tu mambo mengine
yatafuata tena mazuri kutoka PSPF
إرسال تعليق