COSTAL UNION FC KUMBURUZA ALIYEKUWA MFADHILI WAO “BINSLUM” MAHAKAMANI

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema utakwenda mahakamani kuishtaki Kampuni ya Binslum Tyre kutokana na kitendo cha kutengeneza tisheti za Coastal Union zenye nembo ya kampuni Sound na kuwapa bure mashabiki kuingiza nazo kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara wakiwa wamelipiwa na viingilo vya mchezo husika.
Hali hiyo ni kinyume na utaratibu kutokana na kuwa tayari kampuni hiyo ilishajitoka kufadhili timu hiyo na tayari klabu ya Coastal Union ilikwishapata mfadhili mwengine ambayo ni kiwanda cha Kutengeneza Unga Ngano mkoani Tanga cha Pembe Flours Mills.
Kauli hiyo imetolewa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji Kilichoketi mwishoni mwa wiki ambapo kilikuwa na agenda nne za msingi ambazo ni Suala la mshambuliaji wa Coastal Union Danny Lyanga,Utoaji slipi benki,Jezi za Sound,Tarehe ya Uchaguzi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal
Union,Steven Mguto,Katibu Mkuu Kassim El Siagi,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji,Albert Peter Saimu Amiri na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.
Kimsingi suala ambalo lilikuwa gumzo ni suala la kampuni hiyo kuchukua hatua ya kuwavalisha mahsbiki wa Coastal Union jezi pamoja na kuwalipia viingilio vya mechi kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu.
Kama unavyojua kuwa Kampuni ya Binslum Tyres ilikuwa mhisani wetu na sasa hatuko naye na tayari alishapeleka fedha zake kwenye vilabu vingine ikiwemo Mbeya City sasa tunamshangaa kuendelea kufanya biashara ya matangazo kupitia mashabiki wetu kwa kuwapa tisheti za kuvaa bure ikiwemo kuwalipia viingilio kwenye mechi za ligi kuu zinazochezwa Mkwakwani.
Hivyo kutokana na suala hilo tayari uongozi wa Coastal Union umeshamkamata mshabiki mmoja ambaye ni wakala wa kusambaza tisheti hizo kwa mashabiki na kumpeleka polisi na taratibu za kisheria zinaendelea ili kuweza kukomesha vitendo hivyo ambavyo sio vya kiungwana.
Tayari Kampuni ya Pembe Flours Mills ilishasaini mkataba na Klabu ya Coastal Union wa kufadhili kwa kipindi cha mwaka mmoja hivyo Kampuni hiyo kuendelea kufanya matangazo yake kupitia mashabiki hao ni kuvunja utaratibu uliokuwepo.
Hata hivyo tayari Pembe walishatoa jezi 2000 kwa ajili ya kuziuza kwa masabiki mbalimbali wa soka jijini Tanga zilizokuwa na nembo ya pembe na TSN.
Kuhusu suala la Uchaguzi wajumbe wa Kamati hiyo walikubaliana uchaguzi huo ufanyika Novemba 23 mwaka huu ambapo nafasi zitakazojazwa ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo na wajumbe wawili wa kamati ya utendaji
Suala la Utiliaji Sahihi wajumbe walilipendekeza fedha zitumike kwenye matumizi yanayofahamika ikiwemo kuwekwa utaratibu wa wazi kwenye matumizi husika.

Post a Comment

أحدث أقدم