FABREGAS ASEMA EDEN HAZARD NI JIBU LA MESSI


KIUNGO mchezeshaji wa Chelsea Cesc Fabregas amemmiminia sifa kibao mshambuliaji Eden Hazard na kusema huyo ndiyo Lionel Messi wa Chelsea.
Hazard aling’ara na Chelsea msimu uliopita na akawa kwenye kiwango cha hali ya juu kwenye mechi dhidi ya Arsenal weekend iliyopita Stamford Bridge.
Alikuwa ni Mbelgiji huyo ndiye aliyebadili mchezo na kusababisha penalti ambayo aliipiga mwenyewe na kuzaa bao la kwanza la Chelsea.

Akizungumza na Radio Cope kuelekea mechi ya Hispania dhidi Slovakia kwenye kufuzu Euro 2016, Fabregas ndiyo mtu anayeleta tofauti Chelsea.
“Hazard ana uwezo mkubwa wa kuwavuruga wapinzani,” alieleza Fabregas ambaye alijiunga na kikosi cha Mourinho  msimu huu kwa pauni milioni 27.
“Yeye ni kiunganishi kikubwa kwetu kati ya safu ya ushambuliaji na kiungo, ni Messi wetu kwa sababu analeta utofauti.”

Post a Comment

Previous Post Next Post