Mjumbe wa kamati, Kitwana Manara (kushoto)
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo (Oktoba 11 mwaka huu) imesikiliza
malalamiko yaliyowasilishwa mbele yake dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro.
Shauri hilo limesikilizwa na
wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti wake Wakili Jerome
Msemwa. Wajumbe wengine wa kamati hiyo waliosikiliza shauri hilo
lililowasilishwa na TFF ni Kitwana Manara, Kassim Dau na Nassoro Duduma.
Hivyo, Kamati hiyo itakuwa na
mkutano na waandishi wa habari kutangaza uamuzi wake juu ya shauri hilo.
Mkutano huo utafanyika Jumatatu (Oktoba 13 mwaka huu) saa 8 mchana
kwenye ofisi za TFF, Jengo la PPF Tower.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
إرسال تعليق