Kauli ya Mh. Godbless Lema dhidi ya kifo cha mtuhumiwa wa Ugaidi

 1.Tobo la risasi katika hiyo picha Linaonekana tumboni. Je hapo ndipo lilipo ---- la kulia? kwanini wadanganje..?? what are they hiding?.
2.Nani mwenye uwezo wa kuthibitisha makosa ya mtuhumiwa na kukiri kwake kuhusika namatukio ya ugaidi?.
3. Hivi mtu anayekimbia anapigwaje risasi ya tumbo? Alikua anakimbia kinyumenyume au? Maana kama kweli alikua anakimbia angepigwa risasi kwa nyuma kwa maana ya mgongoni si tumboni.

4. Hivi unaweza kumkamata mtuhumiwa wa kulipua mabomu tena anayejua kucheza "karate na judo"halafu umsafirishe bila kumfunga pingu?.
5.Kwa jinsi ambavyo nguvu kubwa ilitumika na Polisi wenyewe na hata Serikali nachama tawala kupotosha juu ya tukio lile la milipuko kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, na kwa jinsi ambavyo Rais Kikwete aligomea wito wa Chadema na makundi mbalimbali ya kijamii wa kumtaka aunde tume ya kijaji (Judiciary commission) kuchunguza mauaji yale, kwa nini tuwaamini polisi kuhusu taarifa namaelezo yao kuwa mtuhumiwa alitoroka akiwa chini ya ulinzi kisha akauawa?.
6. Tukumbuke kuanzia mwanzo jeshi la Polisi na hata Rais hawakuonyesha nia njema katika hili leo hii tuwaamini walikuwa wana nia njema ya kumfikisha mtuhumiwa kwenye mikono ya sheria?.
7. Kifo cha mtuhumiwa katika"Mazingira tata" mikononi mwa watuhumiwa wengine (Maana hata polisi walituhumiwa kuhusika) lazima kitaacha maswali mengi bila majibuTunahitaji jeshi linalotoa huduma (PoliceService). nitakuwa wa mwisho kuamini tukio hili.......
(Godbless Lema).

Post a Comment

أحدث أقدم