Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata mlo nyumbani kwa Balozi
Lucas Mtumbuka (kushoto)wa Shina namba moja eneo la Mkimbizi,
alipokwenda kumtembelea yeye na wananchama wake wakati wa ziara ya
kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya
CCM, Jimbo la Iringa Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kinana akichukua mhogo ambao ni sehemu ya vyakula alivyoandaliwa na balozi
Watoto wakipanda kwenye uzio wa nyumba ili wapate kumuona Kinana alipomtembelea Balozi, Lucas Mtumbuka, eneo la Mkimbizi
Kinana akiingia kwenye ukumbi kuzungumza na wanachama 707 wa kikundi
cha Iringa Masoko Vicoba ambapo aliahidi kuwasaidia kuipata mkopo mkubwa
wa fedha watakazokuwa wanakopeshana.
Kinana akizungumza na madereva wa daladala baada ya kuzindua tawi la
wakareketwa wa CCM, mjini Iringa leo. Tawi hilo lina wanachama 60.
Mama Lishe akimnawisha mikono Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
ambapo yeye na viongozi pamoja na baadhi ya wananchama wa CCM walikwenda
kupata chakula cha mchana kwa mama lishe katika Soko Kuu la Iringa leo.
Kinana akiapata mlo wa mchana kwa mama lishe mjini Iringa leo wakati
wa mapumziko ya ziara ya kuimarisha uhai wa chama.Kulia ni Mwenyekiti wa
CCM WIlaya ya Iringa Mjini, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca
Msambatavangu.
Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati (kushoto) akiwa na viongozi wengine
wa CCM wakipata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, mjini Iringa leo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga (katikati) akiwa na
viongozi wengine wa CCM wakati wa chakula cha mchana kwa mama lishe.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha CCM, Daniel Chongolo, akipata mlo huo wa mchana kwa mama lishe.
Wanahabari ambao baadhi yao wako kwenye msafara wa Kinana wakipata mlo wa mchana kwa mama lishe
Kinana akiondoka baada ya kupata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, katika
Soko la Iringa Mjini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa
Mjini.
Post a Comment