TFF yatoa taarifa ya kikao kuangalia mwenendo wa wadau wa Bodi ya Ligi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA YA KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
ILIYOKUTANA OKTOBA 11, 2014- DAR ES SALAAM*

Kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kimefanyika leo kujadili matukio ya hivi karibuni, hasa
mwenendo wa wadau wa Bodi ya Ligi. Shirikisho linatoa tamko kwa umma kama
ifuatavyo:


1. Kamati ya Utendaaji imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni
mpya za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo inaomba radhi kwa wadau ambao
wameguswa na kusumbuliwa na matukio hayo.

2.Kufuatia matukio hayo, Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya Kamati ya
Utendaji, imefungua mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Damas
Ndumbaro ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi ya Klabu ya Simba. Pia wadau wote waliohusika na upotoshaji huo
wakiwemo wafanyakazi wa TFF na Bodi ya Ligi watashughulikiwa kulingana na
nafasi zao.

3.Kutokana na madai ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu
2014/15, Kamati ya Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi
Kuu siku ya Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana
kuhusu changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla.

4.Kamati ya Utendaji itaendelea kuboresha Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi
(Governing Regulations) ili kuweka uwiano wa utendaji na kuepusha tofauti
kati ya Bodi ya Ligi, vilabu na TFF. Aidha Kamati ya Utendaji itafanya kila
linalowezekana kuboresha ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya Ligi kwa lengo la
kuwa na ligi zinazoendeshwa kisasa (Professional Leagues).


*IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)*

Post a Comment

Previous Post Next Post