Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
chama hicho, Nape Nnauye wakiwa katika mkutano wa hadhara katika Kata ya
Kalenga, Iringa Vijini, walipoanza ziara ya siku sita za kuimarisha
uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2010 pamoja na kusikiliza kero za watu na kuzitafutia ufumbuzi.Katika
mkutano huo Kinana aliitaka Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa
kuwatafutia soko la uhakika wakulima.
Kinana akivishwa vazi la kimila la wazee wa kabila la Wahehe ikiwa ni heshima kwake.
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila baada ya kukabidhiwa mkuki.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka Rehema
Said, wakati alipopokea wanachama wapya kutoka Chadema kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika Kata ya Kalenga. Wanachama wapya 21 wa Chadema
walijiunga na CCM

Kinana akionyesha kadi za Chadema alizokabidhiwa wakati wa mkutano huo

Kinana akiwa amekaa na Chifu Abdul Mkwawa pamoja na wazee wa kimila wa kabila la wahehe.
Kinana akipendeza na vazi la kihehe huku akiwa na mkuki mkononi.
إرسال تعليق