![]() |
| Raia huyu wa kikurdi aangalia mapigano katika mji wa Kobane akiwa katika kijiji cha Mursitpinar, kwenye mpaka wa Uturuki na Syria, Oktoba 6 mwaka 2014. AFP PHOTO / ARIS MESSINIS |
Na RFI
Siku moja baada ya wapiganaji wa Dola la Kiislam kudhibiti maeneo matatu
mashariki mwa Kobane nchini Syria, mapigano yanaendela kurindima
mashariki na kusini mwa mji huo karibu na mpaka wa Syria na Uturuki.
Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria, muungano wa
kimataifa umeendesha usiku wa jumatatu kuamkia leo jumanne mashambulizi
mapya dhidi ya ngome za wapiganaji wa dola la Kiislam.
Ni wiki tatu sasa tangu mapigano kati ya wapiganaji wa Dola la Kiislam
na wapiganaji wa Kiikurdi kuzuka karibu na mpaka wa Syria na Uturuki.
Wapiganaji wa dola la Kiislam wametishia kuudhbiti mji wa Kobane.
Kwa mujibu wa kiongozi wa shirika la kutetea haki zabinadamu nchini
syria, mapigano hayo kati ya wapiganaji wa Dola la Kiislam na wapiganaji
wa kikurdi yameelekea kuwa mashambulizi ya kuvizia kwenye barabara za
mji wa Kobane. Raia wameyahama makaazi yao na kukimbilia katika nchi
jirani ya Uturuki. Kobane ni mji wa tatu unaokaliwa na watu kutoka jamii
ya wakurdi wa Syria.
Hayo yakijiri, Bunge la Uturuki liliiruhusu Alhamisi serikali ya Ankara
kuchukua uamzi wa kutuma majeshi yake nchini Syria na Iraq kwa lengo la
kuendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa dola la Kiislam.
Barani Ulaya, kumekua na uhamasishaji wa haraka na wenye nguvu, hususan
katika nchi za Ufaransa, ujerumani, Ubelgiji, Uholanzi. Denmark na
Norway. Viwanja vya ndege vimefungwa, huku maandamano yakipangwa
kufanyika ili kushinikiza mataifa hayo kupambana vilivyo kwa kuhofia
kutekwa kwa mji wa Kobane na wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr

إرسال تعليق