Muimbaji maarufu wa Jamhuri wa Kidemokrasi ya Kongo, Koffi
Olomide alikamatwa na polisi na kuhojiwa kutokana na kujiita ‘Old Ebola’
(Vieux Ebola) kwenye matangazo ya show yake ijayo.
Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu, jina hilo amepewa na mashabiki
wake na kwamba hawana uwezo wa kuwazuia. Koffi Olomide alilazimika kutoa
maelezo kwa polisi nchini humo.
“Imebidi kufuatilia kwasababu tupo kwenye vita dhidi ya mlipuko wa
Ebola. Ni ujumbe mbaya unaotangazwa,” alisema Mkurugenzi wa Habari na
Mawasiliano wa polisi Colonel Pierrot Mwana-Mputu.
“Ebola, inamaanisha kifo. Ni kama tunapingana na jitihada za jumuiya ya kimataifa kupambana na ugonjwa huo,” alisema.
Polisi waliamuru kuondolewa kwa mabango hayo katika mjini wa Kinshasa. Tayari mwanamuziki huyo ameachiwa.
Hiyo sio mara ya kwanza muimbaji huyo kujipa majina ya utani
yaliyosababisha mzozo. Majina mengine aliyowahi kutumia zamani ni
‘Sarkozy’ na ‘Benedict XVI ambapo kanisa katoliki lilimzuia kutumia jina
hilo.
Hata hivyo imebainika kuwa Koffie anajiita ‘Old Ebola’ kama vita aliyoanzisha dhidi ya JB Mpiana ambaye wamekuwa na uadui.
إرسال تعليق