Lotus kutumia injini za Mercedes

Gari ya timu ya Lotus ya Formula 1
Timu ya Lotus ya magari ya langalanga ya Formula 1 itaondokana na matumizi ya injini za Renault kwenye magari yake na badala yake itatumia injini za kampuni ya Mercedes 2015.
Timu hiyo inamaliza uhusiano wa muda mrefu na kampuni ya Renault na kuingia katika kampuni yenye kutengeneza injini zenye ufanisi mkubwa katika mbio za magari ya Formula 1 ili kujaribu kuimarisha ushindani wake.
Timu ya Lotus ilimaliza katika nafasi ya nne katika mashindano ya constructors ya msimu uliopita lakini imeshuka hadi nafasi ya nane mwaka huu.
Afisa mtendaji mkuu Matthew Carter amesema Lotus wameona mkataba huo kama "hatua moja" mbele kuelekea lengo lao la kushinda mbio hizo.
Timu hiyo yenye makaazi yake Oxfordshire-inachukua nafasi ya mkataba wa timu ya McLaren, ambao wanaanza ushirikiano mpya na timu ya Honda msimu ujao, kama moja ya timu tatu wateja wa Mercedes.
Mkataba huo, unaolezwa kuwa wa muda mrefu, umekuwa ukizungumzwa kwa miezi kadha lakini kutangazwa kwake kulicheleweshwa wakati Lotus ikitatua hali hiyo na kampuni ya Renault, ambao waliingia nao mkataba mpya wa miaka mitatu kabla ya kuanza kwa msimu huu.

Post a Comment

أحدث أقدم