Mwenyekiti
CHADEMA jimbo la kanda ya kati, Tundu Lissu, akihutubia wana CHADEMA na
baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida kwenye viwanja vya Peoples
mjini Singida.Tundu pamoja na mambo mengine, amewahimiza wananchi
kuikataa rasimu ya katiba mpya kwa madai kwamba imechakachuliwa.
Na Nathaniel Limu, Singida
IDADI
ndogo ya wanachama na wasio wanachama wa CHADEMA waliohudhuria mkutano
wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa jimbo la kanda ya
kati, Tundu Lissu, kuzungumza nao, ilimuudhi mgeni huyo rasmi na
kutangaza kwamba viongozi wa CHADEMA Manispaa ya Singida, hawana sifa ya
uongozi.
Tundu
akionyesha kukerwa mno na mahudhurio hayo, alisema wananchi wa mji wa
SIngida kwa kipindi cha miaka sita, hawajapata viongozi wanaowastahiki.
“Haya
maneno yaliyosemwa na viongozi wa CHADEMA manispaa ya Singida, kwamba
wananachi wa mji huu, ni waoga kuhudhuria mikutano ya CHADEMA, ni blaa
blaa tupu na hayana ukweli wo wote. Ningejua hali ingekuwa hivi,
nisingekuja”,alisema kwa masikitiko.Alisema
wananchi wa manispaa ya Singida toka CHADEMA izaliwe, hawajawahi kupata
viongozi wenye uwezo bora wa kuongoza, kuhamasisha na kuwaambia ukweli
wa mambo yanayoendelea.
Akifafanua
zaidi, Tundu alisema wananchi wa manispaa ya Singida, sio waoga
kuhudhuria mikutano ya CHADEMA. Mahudhurio mabovu ya leo, ni matunda ya
maandalizi mabovu yaliyofanywa na viongozi wasio na sifa.
Katika
hatua nyingine, Tundu ambaye ni mbunge wa jimbo la Singida mashariki,
alitumia muda mwingi kumsifia baba wa taifa hayati Julius Nyerere, kwa
kudai kwamba alikuwa ni mtu mwenye akili nyingi na alikuwa mwadilifu na
hakuwa mwizi.
“Mwalimu
Julius alikuwa na hekima kweli kweli, lakini hata hivyo alikuwa si
Mungu, alikuwa binadamu kama mimi na wewe. Alikuwa kiongozi safi huwezi
kumlingansiha na watoto wake hawa (marais waliomfuata)”,alisema.
Baadhi
ya wananchi wa manispaa ya Singida,wakimsikiliza mwenyekiti CHADEMA
jimbo la kanda ya kati na mbunge wa jimbo la Singida mashariki, Tundu
Lissu, wakati akiwahutubia.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Kuhusu
rasimu ya katiba mpya, Tundu alisema rasimu hiyo siyo mpya ni ile ile ya
mwaka 1962, isipokuwa imejaa mapambo mapambo, ili kuwaghilibu wanachi.
“Rasimu
ya katiba ingesema rais hana haki ya kumnyang’anya mtu ardhi, rais ni
binadamu aliyefanya makosa kama binadamu wengine, akikosa ashitakiwe.
Mawaziri wasitokane na wabunge au iondoe nafasi za wakuu wa mikoa na
wilaya. Hiyo ningesema ni rasmu bora kwa usatawi wa watanzania” na
kuongeza;
“Katiba
mpya itakuwa ya ovyo kuliko hii ya sasa. Katiba mpya huko mbele
itatupelekea tupigane vita na wazanzibar.Nionavyo mimi ni kwamba
Wazanzibar hawataipitisha kabisa, nina hofu na huku bara, bara kumejaa
ujinga mwingi, kuna uwezekano mkubwa wa kupitishwa rasimu hii ya katiba
mpya”.
إرسال تعليق