Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akizungumza na wananchi jana wakati
wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika
viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.
Katibu
Mkuu wa Wizaraya Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga akisalimia wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya
wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani
Tabora.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tabora Kudra Mwinyimvua akisalimia wananchi jana
wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika
viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akikata utepe kuashiria uzinduzi
rasmi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana jana mkoani Tabora.Kushoto ni ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.
Sihaba Nkinga,Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bibi. Kudra Mwinyimvua na
wa mwisho kulia ni Mwakilishi wa UNFPA Tausi Hassan.
Baadhi ya Vikundi vya Burudani wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana jana mkoani Tabora.
Baadhi
ya wadau wa wiki ya Vijana wakifuatilia Burudani kutoka kwa Kikundi cha
JKT hakipo pichani jana mkoani Tabora wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani hapa.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akielezea jambo alipotembelea banda
la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana mkoa Tabora mara
baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.Katikati ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.
Sihaba Nkinga na mwisho kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Bibi. Joyce Fissoo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akisikiliza maelezo kuhusu mfumo wa
kuwajengea uwezo Vijana kujitengenezea makampuni yao na kumiliki
Biashara alipotembelea banda la Kampuni ya GODTEC jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akiweka saini katika kitabu cha
wageni katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jana mkoa
Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
Baadhi
ya wananchi wakipata huduma ya upimaji wa afya zao katika banda la
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya jana mkoani Tabora ambapo maadhimisho ya
wiki ya Vijana yanaenedele.
Jonas Kamaleki - MAELEZO
Serikali yaweka Mkakati kupunguza changamoto ya ajira kwa Vijana
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imeweka mkakati kukabiliana na changamoto ya
ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kutenga fedha katika halmashauri mbali
mbali nchini kwa lengo la kusaidia miradi ya vijana.
Hayo yamebainishwa na
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bibi Fatma Mwassa wakati wa sherehe za uzinduzi
wa Wiki ya Vijana mjini Tabora leo (jana). Bibi Fatuma amesema kuwa Mkoa
wa Tabora umetenga jumla ya shilingi 1.8 kwa ajili ya kusaidia miradi
ya vijana.
“Serikali inatambua
changamoto zinazo wakabili vijana ikiwemo ukosefu wa ajira ata hivyo
tumekuwa tukijitahidi kukabiliana nazo ikiwemo kwa kutenga fedha kwa
ajili ya kusaidia vijana ambapo hapa mkoani kwetu jumla ya shilingi
bilioni 1.8 zimetengwa katiak halmashauri zote.” Alisema Bibi. Fatma. Aidha
Bibi Fatma aliongeza kuwa Serikali ipo tayari kusaidia Vijana katika
kuendeleza shughuli zao na kuwataka kuwa wabunifu na wenye dhamira ya
kweli katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mkuu huyo wa Mkoa
amewataka vijana wasitumiwe tu na watu wasioitakia mema nchi bali
wajitambue ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuacha
tabia ya kukaa vijiweni. Pia amewaasa vijana kutojihusisha na mada ya
kulevya. “Msitumike katika kubeba madawa hayo matumboni mwenu au kuyauza reja reja,kataeni kutumikishwa,” alisisitiza Bibi Fatma Mwassa.
Amewataka vijana watumie
fursa zilizopo ili waweze kujiendeleza badala ya kulalamika. Amewaasa
watumie ujana wao vizuri kama alivyoutumia Baba wa Taifa, Hayati Julius
Kambarage Nyerere ambaye tunaadhimisha miaka 15 ya kifo chake. Alisema
Mwalimu aliutumia ujana wake vizuri katika shughuli za kisiasa na
kujipatia heshima kubwa.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga amesema kuwa Wiki ya Vijana imekuwa jukwaa muhimu kwa Vijana
wengi hapa nchini kwani upata fursa ya kukutana na kujifunza kupitia
maonyesho yanayoambatanana maadhimisho hayo.
Bibi. Sihaba aliongeza
kuwa kumekuwapo na matokeo chanya yanayotokana na maadhimisho hayo
ambapo baadhi ya vijana wenye dhamira wemepata kuwa wajasiriamali
kupitia wa kubwa na wakati kupitia maadhimisho hayo.
Wiki ya Vijana
inaadhimishwa ikiwa inatimizwa umri wa miaka 15 tokea ilipoanzishwa
mnamo mwaka 2000 Mkoani Kilimanjaro. Katika Wiki hii Vijana mbalimbali
ujumuika pamoja katika maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu
yanafanyoika mkoani Tabora na yatafikia kilele chake tarehe 14 Oktoba
ambayo ni siku ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na kilele cha mbio za
Mwenge.
إرسال تعليق