Vitalu vya miche ya miti vinavyomilikiwa na Umoja wa Vikundi vya Kijamii wilaya ya Mufindi (UVIKIMU)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumwagia maji vitalu
vya miche ya miti vinavyomilikiwa na Umoja wa Vikundi vya Kijamii wilaya
ya Mufindi (UVIKIMU)
Shamba la chai Ngwazi
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchuma chai pamoja na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye shamba la chai Ngwazi
wilaya ya Mufindi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichuma chai, ambapo alitaka
wakulima wadogo pia wasaidiwe ili kufanikisha kilimo ch chai kwani chai
ikisimamiwa vizuri itasaidia kuinua uchumi wa nchi na kumpatia mkulima
kipato kizuri.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia),Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Iringa Jesca Msambatavangu (katikati) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye wakiwapungia mkono wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye
mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya mkutano Nyololo njia panda.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Jimbo la
Mufindi Kusini ambapo aliwaambia anawapongeza wapinzani kwa kukubali
Katiba iliyopendekezwa na amesema kama walivyotangaza kuwa watashawishi
wapiga kura wasiipigie basi na CCM itawashawishi wapiga kura waipigie .
Mwenyekiti wa CCM Ndugu Jesca Msambatavangu akihutubia wananchi kwenye kiwanja cha mkutano Nyololo njia panda
Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Mendrad
Kigola akiwahutubia wananchi wake wa kata ya Nyololo ambapo alisema
maji bado hayajapatiwa ufumbuzi zinahitajika zaidi ya milioni 800
kutatua tatizo la maji.
Hii gari ya aina yake ilikuwa kivutio kwenye mkutano.
Wananchi wakisikiliza mkutano wakiwa juu ya uzio wa kiwanja cha Nyololo njia panda
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa pamoja na mtoto Meliko
Mpevu,na Afisa wa Chama Makao Makuu Edward Mpogolo(watatu kutoka kulia)
na wadau wengine wa CCM wilaya ya Mufindi wakifuatilia kwa makini
mkutano unavyoendelea.
Wananchi wakisikiliza kwa makini
Wananchi wakishangilia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa jimbo la
Mufindi Kusini ambapo aliwaambia tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa
watumishi wengi wa serikali kumechangia sana kushusha nidhamu na
kutofanya kazi kwa ufanisi ,Katibu Mkuu pia alisema kuwekwe utaratibu
mzuri utakaopunguza malalamiko kwenye utoaji wa vibali vya kuvuna
mbao,pia aliwaambia wananchi wa Mufindi kuwa vijiji 46 vitapata umeme
ikiwa vijiji 35 vitapata kupitia mradi wa Umeme Vijijini (REA) na 11
vitapata kupitia mradi wa Mwenga Hydro.
Josephat
Sebadi Soda aliyekuwa Katibu wa Chadema kata ya Igowole akitangaza
rasmi kurudi CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
mikutano Nyololo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
ambapo yeye pamoja na wenzake 27 wamerudi na kujiunga na CCM
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za Chadem
kutoka kwa aliyekuwa Katibu wa Chadema kata ya Igowole Josephat Sebadi
Soda aliyeamua kujiunga na CCM.
Zaidi ya wanachama wapya 485 wamejiunga na CCM wilaya ya Mufindi.
Wanachama wapya wakila kiapo.
Mzee alishindwa kuvumilia na kuamua kuyarudi
Wasanii wa CCm Band Mufindi wakitoa burudani baada ya mkutano kumalizika.
Wananchi wakiserebuka pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano .
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (katikati)na Katibu wa CCM wilaya ya
Mufindi Miraji Mtaturu (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii
wa bendi ya CCM Band Mufindi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye wakiangalia kasha la albamu ya bendi ya CCM Mufindi ambayo
walizindua albamu inayokwenda kwa jina la ILANI.
إرسال تعليق