Miss
Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu akizungumza machache na waandishi wa
habari. video ya alichokisema Miss Tanzania imepachikwa hapo Chini
Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo
ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji
hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga
alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo
alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo
Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo
ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akionyesha nakala ya cheti cha
kuzaliwa cha Mrembo Sitti Mtemvu alicholetewa na wakazazi wake.
Nakala halisi ya Cheti hicho inayoonyesha Mrembo huyo amezaliwa Mei 31,1991.
“Ukweli ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho hapo kinajielezea,
mkitaka mnaweza kwenda hizo sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema
Sitti. Mtemvu alisema cheti chake cha zamani cha kuzaliwa kilipotea
akidai kuwa ni kutokana na maisha yake ya kusafiri mara kwa mara.
“Kwahiyo ilibidi pale walipohitaji cheti nilete kingine,” alijitetea.
“Sikutegemea hayo maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo,”
alijibu mrembo huyo baada ya waandishi wa habari kumtaka awape ripoti
yoyote ya polisi kuhusiana na kupotea kwa cheti chake cha mwanzo.
Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu.
Sitti alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi kuwa ana mtoto. “Sina mtoto, na mkitaka tunaweza kwenda hospitali sababu naona kama mmekuwa mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya kweli,” alisema.
Akijibu swali la kuonekana kwa passport yake inayoonesha kuwa
alizaliwa mwaka 1989 na huku kwenye cheti alichoonesha kikionesha
amezaliwa May 31, 1991, Sitti alisema:
Sitogusia hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa nakuja kuomba ‘Umiss
Tanzania’ niliombwa cheti cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni
personal life, kwahiyo sidhani hata nyie kama kuna mtu atakuja anachukua
passport yetu, ama driving licence ya kweli au feki na kuiweka kwenye
mtandao kama ni kitu ambacho mngependelea.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited
Hashim Lundenga alisema kuwa nafasi ipo wazi kwa wale wenye mashaka na
umri na maisha ya Sitti kupeleka vielelezo halisi ambavyo watavifanyia
kazi.
“Tukishapata proof tutazifanyia kazi vizuri sana na mwenye haki atapata. Sisi hatuwezi kumvua taji, vitahusika BASATA na wizara husika,” alisema Lundenga.
Kuhusu Sitti kudanganya kuwa na umri wa miaka 18 kama watu walivyodai
ndivyo alivyosema, Lundega alidai kuwa hayo yamezushwa mtandaoni na
kwenye shindano hilo hakuna aliyesema hivyo.
“Unaamini kwamba Sitti ana miaka 18?” alihoji Lundenga. “Sasa kama
huamini yote yametoka kwenye vyombo vya habari. Sisi tunaamini cheti cha
kuzaliwa, sasa kama kuna mtu ana doubt na cheti cha kuzaliwa aende RITA
akafanye uchunguzi wake.”
Sauti hii hapa chini:-
Post a Comment