Waajiriwa wapya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo watakiwa kuwa waadilifu

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiongea kwa msisitizo kuhusu maadili ya Utumishi wa Umma wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasirimali Watu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru akifafanua jambo wakati wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Wizara hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa mikutano uliopo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mwajiriwa mpya katika kada ya Afisa Habari akichangia mada wakati wa semina elekezi ya waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo elekezi kwa ajili ya kuwajengea uwezo kujua taratibu za Kiutumishi wa Umma semina iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waajiriwa wapya na baadhi ya viongozi wa wizara hiyo mara baada ya kufungua mafunzo kwa watumishi wapya leo jijini Dar es Salaam.

Picha na Frank Shija, WHVUM

Post a Comment

Previous Post Next Post