BAADHI
ya vijiji, vimeelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) kujitungia kiholela na kuzitumia sheria zake ndogo kabla
hazijakubalika na kupitishwa kisheria na mamlaka zinazohusika.
Afisa
Takukuru kutoka ofisi ya taasisi hiyo mkoani Iringa, Ismail Bukuku
alisema moja ya sheria ndogo inayotumiwa na baadhi ya vijiji inahusu
kuwatoza faini ya hadi Sh 300,000 wanaume wanaokamatwa wakijihusisha
kimapenzi na wanafunzi hasa wale wa shule za msingi.
Akiwasilisha
mada ya rushwa katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya
wilaya ya Iringa kilichofanyika hivikaribuni mjini Iringa, Bukuku
alisema matumizi ya sheria kama hizo yanaangukia kwenye makosa ya
rushwa.
cdt: bongo leaks
إرسال تعليق