
Ofisa Elimu wilayani Ulanga, Ephraim Simbeye
alisema hayo mjini hapa jana na kuongeza kuwa, Ulanga ni miongoni mwa
wilaya za Morogoro zinazoongoza kwa wanafunzi kukatisha masomo.
Alisema hali hiyo inachangiwa na baadhi ya wazazi
kushindwa kutoa taarifa sahihi za watoto wao, licha ya Serikali
kuendelea na jitihada za kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya
sheria.
Akizungumzia ujenzi wa maabara unaoendelea katika
shule za sekondari za kata, alisema kwa sasa vyumba 14 vimeshakamilika
na 54 vipo katika hatua za mwisho kukamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aliwataka
viongozi wote wa halmashauri hiyo kuhakikisha wilaya hiyo inaongeza kasi
katika ujenzi ili kuendana na agizo la Rais Jakaya Kikwete la kumaliza
ujenzi Novemba 30 mwaka huu.
Alisema ipo haja ya wananchi kuchangia kiasi cha
fedha kinacholingana, lakini kisiwaumize hadi wakashindwa kuchangia
ujenzi wa maabara.
- Mwananchi
- Mwananchi
Post a Comment