400 waacha shule kwa mimba, utoro

Ulanga. Zaidi ya wanafunzi 400 wilayani hapa, mkoani Morogoro wameshindwa kuendelea na masomo ya sekondari kwa kwa sababu mbalimbali, ikiwamo ujauzito na wengine kukimbilia katika biashara ya uchimbaji wa madini.
Ofisa Elimu wilayani Ulanga, Ephraim Simbeye alisema hayo mjini hapa jana na kuongeza kuwa, Ulanga ni miongoni mwa wilaya za Morogoro zinazoongoza kwa wanafunzi kukatisha masomo.
Alisema hali hiyo inachangiwa na baadhi ya wazazi kushindwa kutoa taarifa sahihi za watoto wao, licha ya Serikali kuendelea na jitihada za kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Akizungumzia ujenzi wa maabara unaoendelea katika shule za sekondari za kata, alisema kwa sasa vyumba 14 vimeshakamilika na 54 vipo katika hatua za mwisho kukamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aliwataka viongozi wote wa halmashauri hiyo kuhakikisha wilaya hiyo inaongeza kasi katika ujenzi ili kuendana na agizo la Rais Jakaya Kikwete la kumaliza ujenzi Novemba 30 mwaka huu.
Alisema ipo haja ya wananchi kuchangia kiasi cha fedha kinacholingana, lakini kisiwaumize hadi wakashindwa kuchangia ujenzi wa maabara.
- Mwananchi

Post a Comment

أحدث أقدم